• HABARI MPYA

  Sunday, August 19, 2018

  SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUFUNGA MABAO MAWILI KRC GENK YASHINDA 3-1 UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameendelea kuisaidia timu yake, KRC Genk baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Sporting Charleroi kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji leo Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Samatta alifunga bao la pili dakika ya 77 na la tatu dakika ya 90 na ushei kwa penalti, baada ya beki Mfinland, Jere Uronen kufunga la kwanza dakika ya 45 na ushei, ambalo lilikuwa la kusawazisha kufuatia kiungo Mspaniola, Cristian Benavente kuanza kuifungia Sporting Charleroi dakika ya 27.
  Na alifunga mabao hayo baada ya kuingia uwanjani akitokea benchi kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mbelgiji, Zinho Gano dakika ya 53.

  Kwa ushindi huo, Genk inafikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi nne na kupanda nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo, nyuma ya Anderlecht inayoongoza kwa pointi zake 12.
  Samatta mwenye umri wa miaka 25, yupo katika mwaka wake wa tatu tangu asajiliwe Genk Januari 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vukovic, Uronen, Lucumi, Aidoo, Maehle, Berge, Malinovskyi/Seck dk90+2, Pozuelo, Trossard/Paintsil dk61, Ndongala na Gano/Samatta dk53.
  Charleroi; Riou, Martos, Rezaei (75 'Perbet), Benavente, Marinos, Baby (62' Norafkan), Hendrickx (81 'Fall), Dessoleil, Nurio, Ilaimaharitra and Gholizadeh.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUFUNGA MABAO MAWILI KRC GENK YASHINDA 3-1 UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top