• HABARI MPYA

  Wednesday, August 15, 2018

  OKWI AFUNGA MAWILI SIMBA SC YAICHAPA 2-1 ARUSHA UNITED KIRAFIKI SHEIKH AMRI ABEID

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Arusha United jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
  Huo ni ushindi wa kwanza kwa Simba SC tangu irejee kutoka Uturuki kwenye kambi yake ya kujiandaa na msimu baada ya sare mbili mfululizo, 1-1 na Asante Kotoko mjini Dar es Salaam na 0-0 Nyamungo FC huko Ruangwa mkoani Lindi.
  Katika mchezo wa leo, mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi dakika za saba na 29 wakati bao pekee la AU limefungwa na Ally Kabunda dakika ya 17.

  Baada ya mchezo huo, Simba SC iliyo chini ya kocha Mbelgiji, Patrick J Aussems itaendelea na mazoezi kesho mjini Arusha, kabla ya Ijumaa kupanda ndege kwenda Mwanza ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar Jumapili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKWI AFUNGA MAWILI SIMBA SC YAICHAPA 2-1 ARUSHA UNITED KIRAFIKI SHEIKH AMRI ABEID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top