• HABARI MPYA

  Wednesday, August 15, 2018

  GWIJI WA KOMBE LA FA AFUNGWA MIAKA MIWILI KWA UTAPELI

  MMOJA wa wafungaji wa mabao ya kihistoria katika historia ya michuano ya Kombe la FA England, Ricky George, amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kushiriki mpango wa utakatishaji fedha, Pauni 250,000 na kusababisha waliyemtapeli kupatwa na shinikizo la damu.
  Mwaka 1972 George, ambaye sasa ana umri wa miaka 72, alijipatia umaarufu nchi nzima baada ya bao aliloifungia timu ambayo ilikuwa haishiriki ligi, Hereford United likiisaidia kuitoa timu ya Ligi Kuu, Newcastle United katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Tatu.
  Lakini mwezi uliopita alihukumiwa kifungo katika mahakama ya St Albans Crown Court, baada ya kukutwa na hatia ya utakatishaji fedha, pamoja na mwanawe, Adam mwenye umri wa miaka 40, ambaye pia amefungwa. 

  Gwiji wa Kombe la FA, Ricky George amehukumiwa kifungo miaka miwili jela kwa utakatishaji fedha Pauni 250,000

  Utakatishaji fedha huo, unahusisha uuzaji wa nyumba bila kumshirikisha mwenye mali wakipokea jumla ya Pauni 250,000 na mnunuzi baada ya kugundua ametapeliwa akapatwa na shinikizo la damu.
  Kufuatia mauziano hayo, Adam George akaingiza Pauni 120,000 kwenye akaunti yake ya biashara kwa maelekezo ya baba yake na Pauni 110,000 zilitolewa fedha taslimu kwa mtu wa tatu, Charles Jogi, mwenye umri wa miaka 57 na kupewa mtu asiyejulikana.
  Mahakama iliambiwa kwamba watatu hao walijikuta katika wakati mgumu baada ya kufuja fedha hizo kupitiliza.
  Adam George, wa barabara ya Burleigh, St Albans, amefungwa miezi 15, wakati Jogi, mwenye miaka 57, wa Hill Close, Stanmore, amefungwa kwa saa 200 akifanya kazi malipo na shughuli za kijamii.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GWIJI WA KOMBE LA FA AFUNGWA MIAKA MIWILI KWA UTAPELI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top