• HABARI MPYA

  Monday, August 20, 2018

  RONALDO KUCHUANA NA SALAH, MODRIC TUZO YA ULAYA

  Cristiano Ronaldo atashindana na Mohamed Salah na Luka Modric kuwani tuzo ya Mwanasoka Bora Ulaya 


  WASHINDI WALIOPITA 

  2011 - Lionel Messi
  2012 - Andres Iniesta
  2013 - Franck Ribery
  2014 - Cristiano Ronaldo
  2015 - Lionel Messi
  2016 - Cristiano Ronaldo
  2017 - Cristiano Ronaldo 
  NYOTA Mohamed Salah, Cristiano Ronaldo na Luka Modric wameingia katika orodha ya mwisho ya wachezaji watatu wanaowani tuzo ya Mwanasoka Bora Ulaya wa Mwaka 2017-18 Ulaya, lakini ajabu Lionel Messi ametemwa. 
  Salah ameorodheshwa baada ya kuiwezesha Liverpool kumaliza nafasi ya pili katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.
  Winga huyo wa kimataifa wa Misri alifunga mabao 44 katika msimu wake wa kwanza Liverpool, pungufu ya matatu tu kufikia rekodi ya mfungaji wa mabao mengi kwa msimu moja, Ian Rush. 
  Ronaldo ameteuliwa baada ya kutwaa taji la tano la rekodi la Ligi ya Mabingwa Ulaya - ambalo lilikuwa la tatu mfululizo kwake akiwa na Real Madrid - na kumaliza kama mfungaji bora kwenye michuano hiyo kwa msimu wa sita.
  Na hatimaye, Modric amefurahia msimu mzuri, alioshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya sambamba na kushika nafasi ya pili kwenye Kombe la Dunia na kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano hayo, Mpira wa Dhahabu kwa kuingia kwenye tatu bora ya wawania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Ulaya.
  Lakini ajabu nyota wa Barcelona, Messi hajapata nafasi ya kuingia kwenye tatu bora ya wawania tuzo hiyo baada ya timu yake kutolewa na Roma katika Robo Fainali msimu uliopita.    
  Tuzo hizo huhusisha wachezaji ambao waliong'ata kutoka katika klabu zilizofanya vizuri  kwenye michuano ya Ulaya na nchi na ya nchi wanachama wa UEFA. 
  Nyota hao huchaguliwa kutokana na viwango walivyoonyesha kwenye mashindano yote, kuanzia kwenye Ligi za nchini mwao, bara na kimataifa.


  Lionel Messi hajapata nafasi ya kuingia kwenye tatu bora ya Tuzo ya Mwanasoka Bora Ulaya      

  WALIOINGIA 10 BORA?

  4) Antoine Griezmann – pointi 72
  5) Lionel Messi – pointi 55
  6) Kylian Mbappe – pointi 43
  7) Kevin De Bruyne – pointi 28
  8) Raphaël Varane –  pointi 23
  9) Eden Hazard  – pointi 15
  10) Sergio Ramos – pointi 12
  Orodha hiyo ya wachezaji watatu imechaguliwa na makocha 80 wa klabu zilizoshiriki kuanzia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Europa League msimu uliopita pamoja na Waandishi Habari 50 wanaounda Umoja wa Vyombo vya Habari vya Michezo Ulaya (ESM).
  Wajumbe wa jopo wanachagua orodha yao ya wachezaji watatu, huku kila wa kwanza anapata pointi tano, wa pili pointi tatu na wa tatu pointi moja.
  Orodha hiyo fupi imetajwa leo mchana na mshindi atatangazwa sambamba na droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa mjini Monaco Alhamisi ya Agosti 30, mwaka huu.
  Siku hiyo hiyo, Mchezaji Bora wa Kike wa Ulaya wa Mwaka na na tuzo za Ligi ya Mabingwa Ulaya zitatolewa.    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO KUCHUANA NA SALAH, MODRIC TUZO YA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top