• HABARI MPYA

    Monday, March 19, 2018

    SIMBA SC WAREJEA DAR BAADA YA KUTOLEWA AFRIKA, WAHAMISHIA HASIRA ZAO LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Simba SC kimerejea mjini Dar es Salaam mchana wa leo kutoka nchini Misri, ambako Jumamosi kilitolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua 32 Bora baada ya sare ya 0-0 katika mchezo wa marudiano na wenyeji, Al Masry Uwanja wa Port Said.
    Kwa sare hiyo, Simba SC imetolewa kwa mabao ya ugenini kufuatia sare ya 2-2 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Machi 7.
    Hii inakuwa michuano ya pili Simba kutolewa msimu huu, baada ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) na sasa Simba SC wanaelekeza nguvu zao kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambako wanaongoza.
    Simba SC ina pointi 46 baada ya kucheza mechi 20, wakati mabingwa watetezi, Yanga SC wanafuatia kwa pointi zao 46 pia baada ya kucheza mechi 21, lakini wanazidiwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
    Kwa sasa Ligi Kuu imesimama kwa muda mechi za kimatafa zilizo katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na mechi za Robo Fainali ya Azam Sports Federation (ASFC).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WAREJEA DAR BAADA YA KUTOLEWA AFRIKA, WAHAMISHIA HASIRA ZAO LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top