• HABARI MPYA

    Wednesday, March 21, 2018

    POGBA AWEKA WAZI; NATAKA KUCHEZA PAMOJA NA NEYMAR SIKU MOJA

    KIUNGO wa Manchester UnitedPaul Pogba ambaye kwa sasa hafanyi vizuri ameelezea kiu yake ya kutaka siku moja kucheza na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Neymar.
    Nyota huyo wa United amesema kwamba wakati wa makuzi yake alikuwa anampenda mchezaji wa zamani wa kimataifa wa England, Chris Waddle.
    Pogba, kwa sasa yuko na timu yake ya taifa, Ufaransa inayojiandaa kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Colombia Ijumaa.
    Na katika mahojiano na chaneli ya Televisheni ya Argentina, TyC Sports alionyeshwa kipande cha nukuu ya Neymar akisema: "Napenda namna alivyo na wakati fulani tunaenda kucheza pamoja,".  
    Pogba akajibu kwa kusema: "Ndiyo, Neymar, Neymar. nampenda pia. Pia ana maana ya furaha uwanjani. Kwa Brazil, soka ni kila kitu, ni maisha ya Brazil. Kila mmoja anacheza soka.
    "Napenda kumuona uwanjani anacheza, kwa ujuzi na ufundi wake. Ni staili tofauti. Unaposema neno Neymar duniani, kila mmoja anafahamu huyo ni nani na anafanya nini. Pamoja na hayo kama nitacheza naye siku moja itakuwa safi,"'
    Wakati huo huo, mchezaji huyo wa zamani wa Juventus amesema wakati anaibuka kisoka alikuwa anawapenda wachezaji kama Zinadine Zdane, Lionel Messi, Ronaldinho Gaucho na Ronaldo Lima.

    Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amesema anapenda siku moja kucheza pamoja na Neymar PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    "Nilikuwa nina videos za Maradona. Pele, Chris Waddle, Kaka, wachezaji wengi. Nilitaka kuwa na vitu vua wachezaji wote hao nyota,".
    Kwa sasa Pogba hana wakati mzuri sana Old Trafford na kocha, Jose Mourinho amemkuwa akimtema Mfaransa huyo kwenye mechi kadhaa muhimu. 
    Anatarajiwa kutumia michezo hii ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Colombia na Urusi kurejesha hali yake ya kujiamini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: POGBA AWEKA WAZI; NATAKA KUCHEZA PAMOJA NA NEYMAR SIKU MOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top