• HABARI MPYA

    Saturday, March 31, 2018

    NGORONGORO YAPANIA KUWAZIMA U-20 WA DRC LEO TAIFA

    Na Mwadishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes leo inaanza kampeni za kuwania tiketi ya Fainali za Vijana chini ya umri wa miaka 20, (AFCON) mwaka 2019 kwa kumenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
    Mchezo huo unatarajiwa kuanza Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na utachezeshwa na marefa kutika Uganda, ambao ni William Oloya atakayepuliza kipyenga akisaidiwa na Dick Okello na Issa Masembe.
    Kiingilio cha chini katika mchezo huo wa kwanza wa kufuzu AFCON U20 mwakani nchini Niger kati ya wenyeji Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jumamosi kitakuwa Sh. 1,000.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario  amesema kwamba kiingilio hicho kitahusu majukwaa ya mzunguko tu, wakati majukwaa ya VIP A, B na C watu wataingia kwa Sh. 3,000. 
    Ngorongoro Heroes iliyo chini ya kocha Ammy Conrad Ninje itaingia kwenye mchezo wa Jumamosi ikitoka kushinda mechi mbili za kujipima dhidi ya Morocco 1-0 na Msumbiji 2-1.
    Na kwa ujumla vijana wasiozidi umri wa miaka wa 20 wa DRC na Tanzania watakutana keshokutwa ikiwa ni siku tat utu baada ya kaka zao kukutana na Taifa Stars kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Chui wa Kinshasa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGORONGORO YAPANIA KUWAZIMA U-20 WA DRC LEO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top