• HABARI MPYA

    Monday, March 19, 2018

    LWANDAMINA: HATUTARUDIA MAKOSA, TUTAPAMBANA TUCHEZE MAKUNDI SHIRIKISHO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Yanga SC, Mzambia George Lwandamina amesema kwamba watajitahidi wasirudie makosa ili wakate ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
    “Tunahamia kwenye Kombe la Shirikisho, huko tunakwenda kwa nguvu zote na kiu ya kufanya vizuri baada ya matokeo haya kwenye Ligi ya Mabingwa,”amesema Lwandamina.
    Mzambia huyo amesema anaamini vijana wake wamepata somo baada ya kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa watakuwa makini wasirudie makosa. 
    Yanga SC imetolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Township Rollers Jumamosi Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana.
    Kocha wa Yanga, Mzambia George Lwandamina (kulia) amesema kwamba watajitahidi wasirudie makosa

    Matokeo hayo yanamaanisha Rollers inakwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza historia hiyo kwa ushindi wa jumla wa 2-1 uliotokana na matokeo ya mchezo wa kwanza Dar es Salaam Machi 6.
    Yanga SC sasa wanaangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako watamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. 
    Pamoja na Kombe la Shirikisho, Yanga pia wapo kwenye mbio za mataji mengine mawili nyumbani, Ligi Kuu na Azam Sports Federation Cup (ASFC).
    Katika Ligi wapo nyuma ya Simba SC wanaoongoza pointi 46 baada ya kucheza mechi 20, wakati mabingwa hao watetezi, Yanga SC wanafuatia kwa pointi zao 46 pia baada ya kucheza mechi 21, wakiwa wanazidiwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
    Kwenye Azam Sports Federation Cup Yanga wapo Robo Fainali ambako watamenyana na Singida United Aprili 2, mwaka huu Uwanja wa Namfua mjini Singida.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LWANDAMINA: HATUTARUDIA MAKOSA, TUTAPAMBANA TUCHEZE MAKUNDI SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top