• HABARI MPYA

    Saturday, March 31, 2018

    MKUDE ASAFIRI NA SIMBA SC KWENDA IRINGA KWA AJILI YA MECHI NA NJOMBE MJI JUMANNE

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KIUNGO Jonas Gerald Mkude ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri na kikosi cha Simba SC leo kwenda Iringa kuweka kambi ya kambi siku mbili kabla ya mchezo dhidi ya Njombe Mji FC Jumanne.
    Simba SC watakuwa wageni wa Njombe Mji FC katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe Jumanne.
    Na ka siku mbili kuanzia leo watakuwa Iringa wakifanya mazoezi na kupumzika kwenye hali ya hewa inayoshabibiana na Njombe watakapokwenda Jumatatu.
    Mkude aliumia Jumatatu jioni kwenye mazoezi ya Simba SC Uwanja wa Boko Veterani mjini Dar es Salaam bada ya kugongana na kiungo mwenzake, Muzamil Yassin wakati wa kugombea mpira.
    Jonas Mkude aliumia Jumatatu jioni mazoezini Simba SC Uwanja wa Boko Veterani mjini Dar es Salaam  

    Jitihada za Daktari wa timu, Yassin Gembe kumpatia huduma ya kwanza Mkude hazikumsaidia siku hiyo, kwani hakuweza hata kuukanyagia mguu ulioumia kiasi cha kubebwa kupelekwa kwenye chumba cha kuvalia nguo, kabla ya kurudishwa nyumbani kwa gari.
    Lakini siku iliyofuata tu, Dk. Gembe akasema maumivu ya Mkude hayakuwa makubwa na anaweza kurejea mazoezini baada ya siku tatu.
    Simba wanarejea kwenye Ligi Kuu baada ya kutolewa kwenye Kombe la Shirikisho la Afrika na Al Masry ya Misri kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya 0-0 Machi 17 mjini Port Said na 2-2 Machi 7, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kwenye mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika.
    Simba SC ndiyo wanaoongoza Ligi Kuu kwa wastani wao mzuri wa mabao baada ya kulingana kwa pointi na mabingwa watetezi, Yanga SC 46 kila timu, ingawa pia Wekundu wa Msimbazi wana mechi moja mkononi.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKUDE ASAFIRI NA SIMBA SC KWENDA IRINGA KWA AJILI YA MECHI NA NJOMBE MJI JUMANNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top