• HABARI MPYA

  Tuesday, February 13, 2018

  YANGA YAKUMBANA NA FAINI ‘DABO DABO’ ZA TFF, KILA MOJA NUSU MILIONI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU za Lipuli na Yanga kila moja imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kutumia milango isiyo rasmi kuingia uwanjani katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzaniaq Bara baina yao wiki iliyopita Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, maarufu kama Kamati ya Saa 72 ambayo imesema kitendo hicho ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu na imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
  Aidha, Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutoingia vyumbani, hivyo kwenda kinyume na Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
  Mechi namba 123 (Singida United 3 vs Mwadui 2). Kocha wa makipa wa Mwadui, Lucheke Gaga amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kuondolewa kwenye benchi (ordered off) na Mwamuzi kwa kutoa lugha ya matusi katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 3, 2018 kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 40(11) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.
  Mechi namba 128 (Ruvu Shooting 0 vs Simba 4). Mchezaji wa Ruvu Shooting, Mau Bofu amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kumpiga kiwiko Emmanuel Okwi wa Simba katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 4, 2018 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
  Klabu ya Njombe Mji iliwasilisha malalamiko kuwa Tanzania Prisons ilimchezesha mchezaji James Mwasote katika mechi yao namba 126 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyofanyika Februari 3, 2018 wakati akiwa na kadi tatu za njano.
  Kamati imekataa malalamiko ya Njombe Mji FC kwa vile wakati James Mwasote anacheza mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya alikuwa na kadi mbili za njano. Mwasote alipata kadi hizo kwenye mechi dhidi ya Majimaji na dhidi ya Singida United.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAKUMBANA NA FAINI ‘DABO DABO’ ZA TFF, KILA MOJA NUSU MILIONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top