• HABARI MPYA

  Tuesday, February 13, 2018

  JUMA NYOSO AFUNGIWA MECHI TANO NA FAINI MILIONI MOJA KWA KUMPIGA SHABIKI WA SIMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI wa Kagera Sugar ya Bukoba, Juma Said Nyosso amefungiwa kutocheza mechi tano za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na kutozwa faini ya Sh. Milioni 1 baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga shabiki baada ya mchezo dhidi ya Simba.
  Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Nidhamu iliyokutana Jumamosi Februari 10, 2018 ambacho kilijadili na mambo mengine pia mbali utovu wa nidhamu aliofanya Nyosso kwenye mechi namba 112 ya Ligi Kuu, Kagera Sugar wakifungwa 2-0 na Simba Uwanja wa Kaitaba.
  Juma Nyosso amefungiwa kutocheza mechi tano za Ligi Kuu na kutozwa faini ya Sh. Milioni 1 

  Juma Nyoso alituhumiwa kumpiga shabiki baada ya kumalizika mchezo huo kinyume cha kanuni ya 36 ya ligi Kuu inayozungumzia uchezaji wa kiungwana pamoja na Ibara 50(1)(2) na (5) ya katiba ya TFF toleo la 2015.
  Kamati ilipitia ripoti ya kamishna wa mechi ambayo imeeleza tukio hilo la Juma Nyoso kupishana na shabiki aliyekuwa amebeba vuvuzela  na ndipo Nyoso aliposimama na kuanza kumpiga na kiatu na kutumia goti mpaka askari wa jeshi la Polisi walipoingilia kumuokoa na kumshikilia mchezaji huyo wakati shabiki akipatiwa huduma kwenye gari la huduma ya kwanza.
  Juma Nyoso katika utetezi wake alikana malalamiko dhidi yake akidai kitendo alichofanya ni kukunjana na shabiki.
  Kamati kupitia ripoti ya kamishna wa mchezo huo imemtia hatiani Juma Nyoso kupitia kanuni ya 36 ya kanuni ya Ligi kuu na Ibara ya 50(1)(2) na (5) ya katiba ya TFF.
  Kamati pia ilipokea taarifa za nyuma za nidhamu za Juma Nyoso ambayo rekodi inaonesha aliwahi kufungiwa kwa makosa ya kinidhamu .
  Kupitia kifungu cha 37(10)cha kanuni za ligi Kuu kamati imemtia hatiani Juma Nyoso na imemfungia kutocheza mechi Tano(5) na faini ya Shilingi milioni moja(1,000,000).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JUMA NYOSO AFUNGIWA MECHI TANO NA FAINI MILIONI MOJA KWA KUMPIGA SHABIKI WA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top