• HABARI MPYA

    Wednesday, February 28, 2018

    YANGA SC YAITANDIKA NDANDA FC 2-1 NANGWANDA…MBIO ZA UBINGWA ZAZIDI KUPAMBA MOTO

    Na Mwandishi Wetu, MTWARA
    YANGA SC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
    Ushindi huo unawafanya mabingwa hao watetezi kufikisha pointi 40 baada ya kucheza mechi 19, wakiezidiwa pointi tano na vinara wa Ligi Kuu, Simba SC.
    Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Florentina Zablon wa Dodoma aliyesaidiwa na Abdallah Rashid na Kassim Safisha wa Pwani, hadi mapumziko tayari Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
    Alianza kiungo mshambuliaji Pius Charles Buswita kufunga bao la kwanza dakika ya tano akimalizia kazi nzuri ya kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Papy Kabamba Tshishimbi.
    Beki wa kulia, Hassan Ramadhani Kessy akaifungia bao la pili Yanga SC dakika ya 29 baada ya kuwalamba chenga mabeki wa Ndanda kufuatia pasi ya Buswita aliye katika msimu wake wa kwanza Jangwani tangu asajiliwe kutoka Mbao FC ya Mwanza.
    Yanga ingemaliza kipindi cha kwanza inaongoa kwa mabao 3-0 kama si kiungo Mkongo, Tshishimbi aliyesajiliwa msimu huu kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland kukosa penalti dakika ya 38, ambayo ilipanguliwa na kipa Jeremiah Kisubi kufuatia John Tibar George kuunawa mpira kwenye boksi.
    Kipindi cha pili, Ndanda walio chini ya kocha Malale Hamsini walibadilika na kuanza kupeleka mashambulizi langoni mwa Yanga hadi kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi.
    Bao hilo lilifungwa na Nassor Kapama dakika ya 46 akimalizia kazi nzuri ya kiungo Mrisho Khalfan Ngassa, mchezaji wa zamani wa Fanja ya Oman, Free State Stars ya Afrika Kusini, Yanga, Simba, Azam, Azam FC za Dar es Salaam, Mbeya City, Kagera Sugar na Toto Africans ya Mwanza. 
    Kikosi cha Ndanda FC kilikuwa; Jeremiah Kisubi, William Lucian ‘Gallas’, John Tibar George/Ally Suleiman dk77, Hemedi Khoja, Ahmad Waziri Tajiri/Waziri Majogoro dk40, Jacob Massawe, Majjid Khamis Bakari, Nassor Yahya Kapama, Ahmed Siasa Msumi, Baraka Gamba Majogoro na Mrisho Khalfan Ngassa.
    Yanga SC; Youthe Rostand, Hassan Kessy, Mwinyi Mngwali, Kelvin Yondan, Said Juma ‘Makapu’, Raphael Daudi, Pato Ngonyani, Papy Kabamba Tshishimbi/Geoffrey Mwashiuya dk46, Pius Buswita, Ibrahim Ajib na Emmanuel Martin/Yussuf Mhilu dk86.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAITANDIKA NDANDA FC 2-1 NANGWANDA…MBIO ZA UBINGWA ZAZIDI KUPAMBA MOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top