• HABARI MPYA

    Friday, February 23, 2018

    MASHABIKI WAUA POLISI HISPANIA KABLA YA MECHI YA EUROPA LEAGUE

    ASKARI Polisi wa kikosi cha kuzuia ghasia amefariki dunia baada ya vurugu zilizohusisha mashabiki wa Spartak Moscow na Athletic Bilbao mitaani kabla ya mechi baina ya timu hizo ya Europa League usiku wa Alhamisi.
    Watu wasiopungua watano walikamatwa baada ya vurugu kurushiana mioto, vipeperushi na chupa baina ya mashabiki mjini Bilbao huku wengi wao wakijeruhiwa na kukimbizwa hospitali.
    Polisi mmoja alifariki dunia hospitalini baada ya kupatwa na mshituko wa moyo kufuatia shinikizo la damu. Ofisa huyo alipata pigo usoni kabla ya kupatwa na shinikizo la damu.
    Msemaji wa Polisi ya Basque alisema: "Tunaweza kuthibitisha kifo hiki," lakini kuzungumzia sababu ya kifo hicho.

    Polisi mmoja amefariki dunia baada ya vurugu zilizohusisha mashabiki wa Spartak Moscow na Athletic Bilbao

    Ofisa huyo alifia hospitalini, ambako alipelekwa kufuatia mshituko wa moyo uliosababishwa na shinikizo la damu wakati Polisi wa Basque, Ertzaintza walipokuwa wakijaribu kuzuia mapambano ya mtaani baina ya mashabiki wa timu hizo mbili.
    Katika taarifa yake, UEFA imesema: "UEFA inasikitishwa mno na vurugu zilizojitokeza mjini Bilbao usiku wa Alhamisi,".
    "Tunawasiliana na Mamlaka za pale kupata maelezo zaidi juu ya kilichotokea. UEFA inatuma salamu za rambirambi kwa familia na jamaa wa Afisa Polisi aliyefariki dunia,".
    Mashabiki wapatao 2,500 wa Urusi walitarajiwa kusafiri kwenda Hispania kwenye mechi na Bilbao na kusababisha ulinzi mkubwa ambao haujawahi kutokea katika Jiji hilo.
    Lakini ulinzi huo haukutosha kuzuia vurugu zilizojitokeza mitaani hadi kusababisha kifo cha askari huyo. 
    Kiasi cha askari Polisi 700 na walinzi wengine 200 wa kampuni binafsi inaelezwa walikuwa mjini Bilbao na Uwanja wa San Mames kujaribu kuzuia vurugu.
    Spartak imetolewa kwenye Europa League usiku wa jana licha ya kushinda 2-1, kwani mechi ya kwanza walifungwa 3-1 nchini Urusi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MASHABIKI WAUA POLISI HISPANIA KABLA YA MECHI YA EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top