• HABARI MPYA

  Friday, February 16, 2018

  YANGA KUWAFUATA SAINT LOUIS JUMAPILI NA HESABU KALI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Yanga SC kinatarajiwa kuondoka Jumapili mchana kwenda mjini Victoria nchini Shelisheli kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Saint Louis Suns Jumatano.
  Lakini wachezaji wanne, beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na washambuliaji watatu, mzawa Yohanna Oscar Nkomola, Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma hawatasafiri kwa sababu wote bado majeruhi.
  Pamoja na hayo, kocha Mzambia, George Lwandamina anajivunia kikosi chake kipana kinachojumuisha wachezaji chipukizi ambao wamekuwa wakiibeba timu katika wakati mgumu.
  Papy Kabamba Tshishimbi alifunga mabao mawili Yanga ikishinda 4-1 dhidi ya Maji Maji 

  Mchezo wa kwanza Yanga ilishinda 1-0 Jumamosi iliyopita, hivyo inakabiliwa na mtihani mgumu wa kwenda kushinda ugenini, au kulazimisha sare.
  Yanga ilionekana kufanyia kazi makosa yake baada ya Jumatano kushinda 4-1 dhidi ya Maji Maji ya Songea katika mchezo uliofuata wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa.
  Nyota wa mchezo wa siku hiyo alikuwa kiungo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Papy Kabamba Tshishimbi aliyefunga mabao mawili, moja kila la kipindi, la kwanza na la mwisho wakati mabao mengine yalifungwa na Emmanuel Martin naq Obrey Chirwa.
  Tshishimbi alifunga kwa penalti dakika ya 18 na la nne dakika ya, Chirwa dakika ya 29 na Emmanuel Martine dakika ya 43, wakati la Maji Maji lililofungwa na Geoffrey Mlawa dakika ya 56.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUWAFUATA SAINT LOUIS JUMAPILI NA HESABU KALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top