• HABARI MPYA

  Friday, February 16, 2018

  LIPULI NA AZAM FC HAKUNA MBABE SAMORA, SARE 0-0

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA
  TIMU ya Azam FC imezidi kujitoa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Lipuli FC Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Matokeo hayo, yanaifanya Azam FC ijiongezee pointi moja na kufikisha 35 baada ya kucheza mechi 19 ikiendelea kukamata nafasi ya tatu, nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 37 na vinara, Simba SC wenye pointi 42 ambao wote wamecheza mechi 18.
  Kwa Lipuli iliyorejea Ligi Kuu msimu huu baada ya karibu miaka 20, wanafikisha pointi 20 katika mechi ya 19 na kupanda hadi nafasi ya saba, ikizishusha Mbao FC na Ruvu Shooting, ambazo zina mechi moja moja mkononi.    
  Ligi Kuu inatarajiwa inatarajiwa kuendelea kesho kwa mechi mbili, Njombe Mji FC wakiwakaribisha Maji Maji Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe na Kagera Sugar wakiwa wenyeji wa Singida United, Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja tu, Mbeya City wakiikaribisha Stand United Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, wakati Jumatatu Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Mwadui FC Uwanja wa Sokoine na Mtibwa Sugar wataikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
  Kikosi cha Lipuli FC kilikuwa; Mohammed Yussuf, Sylvester Mganga, Emmanuel Kichiba, Novaty Lufunga, Ally Mtoni, Abeid Tangaru, Shaaban Ada/Seif Karihe dk75, Zawadi Mauya/Omega Seme dk81, Adam Saramba, Malimi Busungu na Jamal Mnyate.
  Azam FC; Razack Abalora, Saleh Abdallah, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Joseph Mahundi, Salmin Hoza, Yahya Zayed/Mbaraka Yussuph dk84, Shaaban Iddi, Iddi Kipwagile. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIPULI NA AZAM FC HAKUNA MBABE SAMORA, SARE 0-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top