• HABARI MPYA

  Sunday, February 18, 2018

  SAMATTA ALIMWA KADI YA NJANO GENK IKILAZIMISHA SARE YA 2-2 UGENINI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana alionyeshwa kadi ya njano timu yake ikilazimisha sare ya 2-2 na wenyeji, Club Brugge katika mchezo wa Ligi Daraja La Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Jan Breydel mjini Brugge.
  Samatta alionyeshwa kadi hiyo dakika ya 87, zikiwa ni dakika 15 tangu aingie uwanjani kutokea benchi kuchukua nafasi ya ya Nikolaos Karelis.
  Katika mchezo huo, Karelis aliondoka uwanjani akiwa amekwishaifungia Genk bao la kuongoza dakika ya 11, kabla ya Vanaken kuwafungia wenyeji mabao mawili la kwanza kwa penalti 14 na lingine dakika ya 63.
  Mbwana Samatta jana alionyeshwa kadi ya njano, KRC Genk ikilazimisha sare ya 2-2 na wenyeji, Club Brugge 

  Baada ya Samatta kuingia akaenda kuisaida Genk kupata sare ya ugenini, kwani Malinovskyi aliisawazishia kwa penalti dakika ya 84.
  Samatta jana alicheza mechi ya 76 tangu alipojiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Na katika mechi hizo, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.
  Kikosi cha Club Brugge kilikuwa: Vermeer, Scholz, Wesley, Diaby/Dennis dk73, Mitrovic, Limbombe, Vanaken, Cools, Vormer, Nakamba na Mechele.
  KRC Genk : Vukovic, Nastic, Colley, Aidoo, Mata, Wouters, Seck, Malinovskyi, Pozuelo/Writers dk91, Ndongala/Buffalo dk73 na Karelis/Samatta dk72.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ALIMWA KADI YA NJANO GENK IKILAZIMISHA SARE YA 2-2 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top