• HABARI MPYA

  Saturday, February 17, 2018

  ROBO FAINALI FA; MAN UNITED NA BRIGHTON, CHELSEA NA LEICESTER

  Mabingwa mara 12 wa Kombe la FA England, Manchester United watamenyana na Brighton katika Robo Fainali PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  RATIBA YA ROBO FAINALI KOMBE LA FA

  Sheffield Wednesday/Swansea vs Rochdale/Tottenham
  Manchester United vs Brighton 
  Leicester vs Chelsea
  Wigan/Manchester City vs Southampton 
  MABINGWA mara 12 wa Kombe la FAManchester United watamenyana na Brighton katika Robo Fainali ya michuano huyo.
  Chelsea watasafiri kuwafuata Leicester katika mechi nyingine ya robo fainali itakayozikutanisha timu za Ligi Kuu tupu.
  Sheffield Wednesday au Swansea mojawapo itamenyana na Rochdale au Tottenham wakati Wigan au Manchester City itakuwa mwenyeji wa Southampton.  
  Timu kubwa za Ligi Kuu ya England zimefanikiwa kukwepa mechi baina yao kwa wao katika hatua ijayo. 
  Pamoja na hayo, Leicester, iliyoifunga Sheffield United 1-0 Ijumaa itakutana na mtihani mzito wa kikosi cha Mtaliano, Antonio Conte wa Chelsea Uwanja wa King Power.
  The Blues yenyewe iliitupa nje timu ya Daraja la Kwanza England, maarufu kama Championship, Hull 4-0 usiku wa Ijumaa. Mechi za Robo Fainali zitachezwa kuanzia Machi 16 hadi 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROBO FAINALI FA; MAN UNITED NA BRIGHTON, CHELSEA NA LEICESTER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top