• HABARI MPYA

  Wednesday, February 14, 2018

  MAJI MAJI WAIFUATA YANGA NA KIBURI, MECHI KUPIGWA LEO DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Maji Maji ya Songea, Habib Kondo amesema haihiofii Yanga SC kuelekea mcheoz wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Kondo amesema kwamba anachojua Yanga watakuwa wanacheza nyumbani katika mazingira waliyozoea, lakini wao Maji Maji wamejiandaa kwa hilo.
  “Tunatarajia utakuwa mchezo mgumu kwa sababu Yanga ni timu kubwa ina mashabiki wengi na wana malengo ya kutetea ubingwa wao, lakini sisi tumekuja hapa kufuata pointi tatu, hivyo nasi tunataka ushindi. Utakuwa mchezo mgumu,”amesema.
  Maji Maji ya Songea leo inakabiliana na mabingwa watetezi, Yanga mjini Dar es Salaam 
  Kocha wa Maji Maji, Habib Kondo amesema hawaihofii Yanga kuelekea mchezo wa leo

  Kwa upande wake, kocha Msaidizi wa Yanga, Nsajigwa Shadrack amesema kwamba wanatarajiwa kuingia katika mchezo mwingine mgumu, lakini watajitahidi washinde leo ili kujiweka katika mazingira mazuri.
  Mchezo wa kwanza baina ya Maji Maji na Yanga Uwanja wa Maji Maji mjini Songea ulimalizika kwa sare ya 1-1 na leo timu zinakutana katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
  Huu ni mchezo wa kiporo ambao ilikuwa ufanyike Jumamosi, lakini ukasogezwa mbele kwa sababu Yanga walikuwa wanacheza mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Saint Louis Suns United siku hiyo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kushinda 1-0.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mchezo mmoja wa kiporo pia, vinara Simba SC wakiwa wageni wa Mwadui FC Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAJI MAJI WAIFUATA YANGA NA KIBURI, MECHI KUPIGWA LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top