• HABARI MPYA

  Friday, February 16, 2018

  LIVERPOOL, MAN UNITED NA CHELSEA ZAMFUATILIA WANYAMA

  KLABU ya Liverpool inafuatilia maendeleo ya kiungo Mkenya wa Tottenham Hotspur, Victor Wanyama.
  Manchester United na Chelsea zimegundua pia kwamba mwanasoka huyo wa kimataifa wa Kenya anambeba kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino baada ya kurejea kutoka kwenye maumivu.
  Wanyama alianzishwa kwenye mechi za Kombe la FA dhidi ya AFC Wimbledon na Newport County, lakini kwenye mechi nyingine nane amekuwa akiingizwa kutokea benchi baada ya kupona maumivu ya goti.
  Hiyo ni pamoja na dakika 12 za mchezo dhidi ya Liverpool alipoingia na kubadilisha mchezo katika sare ya 2-2.

  Liverpool inafuatilia maendeleo ya kiungo wa Tottenham, Mkenya Victor Wanyama PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Nahodha wa zamani wa Anfield na sasa kocha wa timu ya vijana, Steven Gerrard amegusia kwamba Liverpool inahitaji kutafuta kiungo mzuri wa ulinzi ili kuwaongezea nguvu wachezaji wapya watarajiwa, Naby Keita na Jordan Henderson.
  Na kutokana na taarifa za Emre Can kuhamia Juventus mwishoni mwa msimu, Gerrard amesema: "Nafikiri Liverpool itanufaika na kiungo mzuri wa ulinzi, mzuiaji. Mchezaji aina ya Wanyama, ambaye anajituma, ana nidhamu na atakayempa ulinzi zaidi beki namba nne,".
  "Kuondoka kwa Emre Can, wazi Keita anaingia. Lakini Keita ni namba nane (8), Keita anatembea na mpira, na anakimbia.
  "Kwa namna (Klopp) anavyotumia mfumo wa 4-3-3 itafaa zaidi. Hivyo unaweza kuwapanga Henderson na Keita.'
  Pamoja na hayo, Gerrard anaonekana kumtaka zaidi, Wanyama akimuelezea kama mchezaji wa dhamira na anayewajua wachezaji kadhaa wa Liverpool tangu akiwa Southampton.
  Manchester United na Chelsea nazo pia zimekuwa zikimfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. Kocha Mtaliano wa Chelsea, Antonio Conte amemtaja Wanyama kama mmoja wa wachezaji tegemeo wa Tottenham.
  "Kuna mchezaji ambaye ni muhimu mno kwa sasa kwao, Wanyama,"alisema Conte msimu uliopita. "Ni mchezaji mzuri haswa. Ana ubora wakati wa mechi, stamina, anajituma na anajitolea kwa ajili ya timu. Napenda vitu hivyo juu yake,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL, MAN UNITED NA CHELSEA ZAMFUATILIA WANYAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top