• HABARI MPYA

    Saturday, December 02, 2017

    ULIMWENGU ANAJIFUA VIKALI ILI AREJEE UWANJANI FITI ZAIDI

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu anaendelea vizuri na mazoezi ya kujiandaa kurejea uwanjani baada ya kuumia Julai mwaka huu katika klabu yake ya AFC Eskilstuna ya Sweden.
    Ulimwengu yuko katika mazoezi makali hivi sasa kuanzia gym, ufukweni na kuchezea mpira kidogo akiwa peke yake baada ya kupata ahueni ya maumivu yake. 
    Hiyo ni baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti katika hospitali ya Taasisi ya Sayansi ya Michezo mjini Cape Town, Afrika Kusini.
    Maumivu ya goti yamekuwa yakimsakama Ulimwengu tangu alipojiunga na Eskilstuna Januari mwaka huu akitokea Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kiasi cha kushindwa kucheza. 
    Thomas Ulimwengu anaendelea vizuri na mazoezi ya kujiandaa kurejea uwanjani baada ya kuumia Julai mwaka huu 

    Ulimwengu aliyezaliwa Juni 14, mwaka 1993 aliibukia katika taasisi ya soka Tanzania (TSA) mwaka 2008, kabla ya mwaka 2009 kwenda kuanza kukomazwa Ligi Kuu katika klabu ya Moro United alikokuwa akicheza kwa mkopo hadi mwaka 2010 alipokwenda akademi ya AFC Eskilstuna ya Sweden, alikocheza hadi mwaka 2011  alipochukuliwa na timu ya vijana ya Mazembe.
    Alicheza U-20 ya Mazembe kwa msimu moja kabla ya kupandishwa rasmi timu ya wakubwa mwaka 2012 na moja kwa moja kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza hadi anamaliza Mkataba wake Oktoba mwaka jana.
    Ulimwengu alihamia Ulaya baada ya kushinda mataji makubwa akiwa na  Mazembe kama Ligi ya Mabingwa Afrika, Super Cup ya Afrika na pamoja na kucheza Klabu Bingwa ya Dunia. Ingawa hajaweka wazi, lakini kuna uwezekano Ulimwengu akaondoka Sweden na kwenda Ubelgiji au Iceland.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ULIMWENGU ANAJIFUA VIKALI ILI AREJEE UWANJANI FITI ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top