• HABARI MPYA

  Friday, December 01, 2017

  MARADONA AIWEKA ENGLAND PAMOJA NA TUNISIA, UBELGIJI KOMBE LA DUNIA 2018 URUSI

  MAKUNDI YOTE KOMBE LA DUNIA 2018 URUSI
  Kundi A; Urusi, Saudi Arabia, Misri na Uruguay 
  Kundi B; Ureno, Hispania, Morocco na Iran 
  Kundi C; Ufaransa, Australia, Peru na Denmark
  Kundi D; Argentina, Iceland, Croatia na Nigeria 
  Kundi E; Brazil, Uswisi, Costa Rica na Serbia 
  Kundi F; Ujerumani, Mexico, Sweden na Korea Kusini
  Kundi G; Ubelgiji, Panama, Tunisia na England 
  Kundi H; Poland, Senegal, Colombia na Japan 

  Gwiji wa soka wa Argentina, Diego Maradona akiinua karatasi ya England kuipanga pamoja na Ubelgiji, Tunisia na Panama katika Kundi G kwenye kombe la Dunia mwakani nchini Urusi PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  GWIJI wa soka wa Argentina, Diego Maradona ameinua karatasi ya England na kuiweka katika Kundi G kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi.
  Katika zoezi la upangaji makundi na ratiba ya michuano hiyo lililofanyika leo Kremlin mjini Moscow, nyumbani kwa wenyeji, Urusi, England itamenyana na Ubelgiji, Tunisia na Panama kuwania kwenda hatua ya mtoano katika fainali za Kombe la Dunia mwakani Urusi.
  Kundi B linakutanisha majirani, Hispania na Ureno ambao watamenyana na Iran na Morocco katika mechi za ufunguzi, wakati mabingwa watetezi, Ujerumani wamepangwa Kundi F na wataanza kutetea taji dhidi ya Mexico, kabla ya kuvaana na Sweden kisha Korea Kusini. 
  Mechi ya kwanza kabisa ya Iceland katika Kombe la Dunia itakuwa dhidi ya Argentina, kufuatia timu hiyo iliyoisumbua England katika Euro 2016 kupangwa na washidi hao mara mbili wa michuano hiyo katika Kundi D. 
  Nigeria imepangwa kundi hilo hilo pamoja na timu ya Lionel Messi kwa mara ya tano kwenye fainali sita. Croatia ni timu nyingine kwenye kundi hilo.
  Mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya Urusi dhidi ya Saudi Arabia mjini Moscow, ambazo zimepangwa pamoja Kundi Kundi A na Misri na Uruguay. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MARADONA AIWEKA ENGLAND PAMOJA NA TUNISIA, UBELGIJI KOMBE LA DUNIA 2018 URUSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top