• HABARI MPYA

  Friday, December 01, 2017

  KUELEKEA MECHI NA ARSENAL; POGBA HAPENDI 'KUPAKI BASI'

  KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba amesema kwamba hapendi mchezo wa kujihami — bali anapenda mchezo wa kumiliki zaidi mpira.
  Manchester United wanakamilisha mipango yao kuelekea mechi kali ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Arsenal, lakini Pogba amesema kwamba mchezo wa kujihami ni tofauti na aliofundishwa.
  "Aina ya mchezo ninaoupenda ni wa kumiliki mpira mwanzo mwisho," amesema mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa. "Mchezo mbaya, nafikiri ni ule ule kwa kila mmoja – kucheza bila mpira,".
  "Kujilinda bila kuwa na mpira kwa sababu unatakiwa kuzunguka ukiwa huna mpira, wakati wote nimejifunza kucheza na rafiki zangu,"amesema.

  Nyota wa Manchester United, Paul Pogba amesema kwamba hapendi mchezo wa kujihami PICHA ZAIDI GONGA HAPA


  Pogba anaamini Arsenal watamkosa Mfaransa mwenzake, Alexandre Lacazette katika mechi ya Jumamosi.
  Kocha wa Gunners, Arsene Wenger amethibitisha wapinzani wao hao wa London Kaskazini watamkosa mshambuliaji wao huyo nyota kesho Uwanja wa Emirates.
  Na Pogba amesema hizo zinaweza kuwa habari njema kwa kikosi cha Jose Mourinho wakifukuzuia ushinid wa nne mfululizo kwenye Ligi Kuu ya England wikiendi hii.
  United watakwenda kwenye mchezo huo wakitoka kushinda 4-2 dhidi ya Watford katikati ya wiki, shukrani kwake Ashley Young aliyefunga mabao mawili.
  United wamefanya mazoezi yao ya mwisho leo viwanja vya Carrington kabla ya safari ya London kwa ajili ya mchezo huo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KUELEKEA MECHI NA ARSENAL; POGBA HAPENDI 'KUPAKI BASI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top