• HABARI MPYA

  Monday, December 11, 2017

  HATUA YA MAKUNDI CHALLENGE YAKAMILISHWA LEO, ZANZIBAR NA LIBYA, BARA NA KENYA

  Na Mwandishi Wetu, MACHAKOS
  HATUA ya makundi ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge inayoendelea nchini Kenya, inatarajiwa kukamilishwa leo kwa michezo mitatu.
  Saa 8:00 mchana, Zanzibar watamenyana na Libya Uwanja wa Jomo Kenyatta, Machakos mchezo ambao utafuatiwa na mechi kati ya wenyeji, Kenya dhidi ya vibonde, Tanzania Bara Saa 10:00 jioni, zote zikiwa mechi za Kundi A, wakati Uwanja wa Kakamega kutakuwa na mchezo mmoja wa Kundi B kati ya Sudan Kusini na Burundi kuanzia Saa 9:00 Alasiri. 
  Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Ammy Ninje ambaye amesema hataki kuondoka Kenya na pointi moja pekee bali angalau washinde na kupata pointi nne.
  Amesema wengi wanauchukulia mchezo huo ni kama wa kukamilisha ratiba, lakini kwao wanaingia kwa nia ya kushinda kwa sababu ni mechi ya ushindani na kila anayecheza anahitaji kushinda.
  “Pamoja na kwamba tumeshatolewa na wengi wanachukulia kesho ni kukamilisha ratiba, sisi tunakwenda kwenye mchezo wa kesho kwa nia ya ushindi kwa sababu tunataka tutoke angalau na pointi zaidi ya hiyo moja tuliyokuwa nayo kwa hiyo tutaingia kupambana kupata ushindi,” amesema Ninje.
  Kilimanjaro Stars itaendelea kuwakosa beki wa kati Kelvin Yondan ambaye bado ana maumivu ya kifundo cha mguu na Mbaraka Yusuph aliyepata majeraha ya misuli.
  Kilimanjaro Stars ipo mkiani mwa Kundi A wakiwa na pointi moja waliyoipata kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Libya ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.
  Zanzibar wanaongoza kundi hilo A wakiwa na pointi saba wakifuatiwa na Kenya wenye pointi tano, Rwanda wenyewe wana pointi nne wakati Libya wana pointi tatu na katika Kundi B ni Uganda na Burundi zinazoelekea kwenda Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HATUA YA MAKUNDI CHALLENGE YAKAMILISHWA LEO, ZANZIBAR NA LIBYA, BARA NA KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top