• HABARI MPYA

  Friday, December 15, 2017

  NGASSA AACHANA NA MBEYA CITY, ATUA NDANDA FC

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  KIUNGO mshambulijai wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa ameachana na Mbeya City baada ya mwaka mmoja kufuatia kumaliza mkataba wake na anaweza kuibukia Ndanda FC ya Mtwara.
  Ngassa ni kati ya wachezaji wawili walioondoka Mbeya City wakati dirisha dogo la usajili likifungwa jana na habari zinasema anaweza kuhamishia maisha yake Mtwara. 
  Ngassa alijiunga na Mbeya City Desemba 15 mwaka jana akitokea Fanja SC ya Oman, aliyodumu nayo kiwa mwezi mmoja na ushei.
  Ngassa alijiunga na Fanja Septemba 21, mwaka jana kwa mkataba wa miaka miwili akitokea ya Free State Stars, alikoondoka Agosti mwaka huo baada ya kuomba mwenyewe kuvunja Mkataba kama ilivyokuwa Fanja.
  Ngassa alijiunga na Free State Stars Mei mwaka 2015 akisajiliwa na kocha Mmalawi, Kinnah Phiri kwa mkataba wa miaka minne.  Hata hivyo, kocha aliyemsajili baba huyo wa Farida (9) na Faria (7) alifukuzwa baada ya miezi miwili tu.
  Katika kipindi cha mwaka mmoja wa kuwa Free State, Ngassa alifanya kazi na makocha wanne akiwemo huyu wa sasa, Mfaransa Denis Lavagne aliyeanza kazi Juni mwaka jana.
  Wengine ni Mjerumani Ernst Middendorp aliyefanya kazi kati ya Septemba na Desemba 2015, Mtaliano Giovanni Solinas aliyefanya kazi kati ya Desemba na Mei 2016.
  Ikumbukwe, Ngassa kisoka aliibukia Toto African ya Mwanza kabla kwenda Kagera Sugar ya Bukoba, Yanga SC, Azam FC na Simba
  Kabla ya kwenda Afrika Kusini alichezea Yanga tena, klabu ambayo inaaminika ni kipenzi cha roho yake.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA AACHANA NA MBEYA CITY, ATUA NDANDA FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top