• HABARI MPYA

    Thursday, May 04, 2017

    TFF YASAINI MKATABA NA WILD AID TANZANIA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi leo amesaini mkataba wa ushirikiano na taasisi binafsi ya Wild Aid Tanzania inayojihusisha na kupiga vita ujangili dhidi ya wanyama pori.
    Katika shughuli hiyo fupi iliyofanyika asubuhi ya leo ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Courtyard, Oysterbay, Dar es Salaam, Malinzi alisema ushirikiano huo utaanza kufanyiwa kazi kupitia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi akibadilishana mikataba na Ofisa wa Wild Aid Tanzania, Lily Massa 


    “Kama mnavyofahamu, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, pamoja na kupromoti, moja ya majukumu makubwa ya TFF ni matatu, kuendeleza, kupromoti na kuongoza mchezo kwa mujibu wa sharia, lakini upande wa jamii huwa pia tunapenda kujihusisha na mambo mbalimbali,”amesema.
    Malinzi amesema huo ni mwendelezo wa mahusiano mazuri kati ya TFF na Jamii na Wild Aid itautumia mpira wa miguu kikamilifu katika kampeni zake za kutunza wanyama pori.  
    Kwa upande wake, Ofisa wa Wild Aid Tanzania, Lilly Massa amesema kwamba wamefurahi kwa kuingia kwenye mahusiano na TFF na mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla.
    Alisema tayari wapo mahusiano na mchezaji nyota wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet anayecheza Marekani na mwanamuziki Ali Kiba hivyo kuongezeka kwa TFF ni hatua nyingine nzuri kwao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YASAINI MKATABA NA WILD AID TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top