• HABARI MPYA

  Thursday, May 04, 2017

  MBARAKA YUSSUF: CHIPUKIZI MWENYE NDOTO ZA KUFIKA MBALI KISOKA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MIONGONI mwa wachezaji wanaofanya vizuri msimu huu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ni mshambuliaji chipukizi, Mbaraka Yussuf Abeid wa Kagera Sugar ya Bukoba.
  Huyo ni mfungaji wa bao la ushindi la timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ikiilaza 2-1 Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Machi 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambaye anawania ufungaji bora wa Ligi Kuu kwa sasa akichuana na Simon Msuva wa Yanga na Shiza Kichuya wa Simba.
  Hivi karibuni, Bin Zubeiry Sports – Online ilifanya mahojiano na mchezaji huyo aliyeibukia katika kikosi cha timu ya vijana cha Simba mjini Dar es Salaam, kabla ya kwenda Bukoba. Endelea.
  Mbaraka Yussuf (kulia) akiwatoka mabeki wa Simba Aprili 2, mwaka huu Uwanja wa Kaitaba, Bukoba 
  Bin Zubeiry Sports – Online: Mambo vipi straika
  Mbaraka Yussuf Abeid: Safi tu bro, karibu
  Bin Zubeiry Sports – Online: Asante, nimekuja kwa ahadi yetu ya mahojiano. Uko tayari?
  Mbaraka Yussuf Abeid: Hakuna shaka, tuendelee tu kaka.
  Bin Zubeiry Sports – Online: vipi mkataba wako unaisha lini Kagera Sugar                        
  Mbaraka Yussuf: Mwisho wa msimu huu
  Bin Zubeiry Sports – Online: Ina maana umebakiza miezi michache tu                        
  Mbaraka Yussuf: Yah                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Vipi Simba una mkataba nao wowote?
  Mbaraka Yussuf: Hapana                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Yanga wakikutaka vipi
  Mbaraka Yussuf: Mimi nipo tayari kucheza timu yoyote kama wakinikidhia mahitaji yangu               
  Bin Zubeiry Sports – Online: Una uhusiano wowote na kipa wa zamani wa Pamba ya Mwanza, Yussuf Abeid
  Mbaraka Yussuf: Hapana.
  Bin Zubeiry Sports – Online:  Baba yako yuko wapi
  Mbaraka Yussuf: Kafariki                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Pole sana. Lini?                        
  Mbaraka Yussuf: Tangu mwaka 2010                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Alikuwa anaishi wapi 
  Mbaraka Yussuf: Kinondoni
  Bin Zubeiry Sports – Online: Kwa hiyo wewe umezaliwa Dar es Salaam?                        
  Mbaraka Yussuf: Yah                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Ulizaliwa lini                         
  Mbaraka Yussuf: Septemba 2 mwaka 1997                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Shule ya Msingi umesoma wapi
  Mbaraka Yussuf: Kumbukumbu                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Sekondari                        
  Mbaraka Yussuf: Nilianzia Tabata, Nikahamia Kinondoni Muslim
  Bin Zubeiry Sports – Online: Umesoma hadi kidato cha ngapi
  Mbaraka Yussuf: Cha nne tu
  Bin Zubeiry Sports – Online: Soka ulianzia wapi 
  Mbaraka Yussuf: Kinondoni Muslim                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Timu ya kwanza ya mtaani kuchezea ni ipi?                        
  Mbaraka Yussuf: Vijana Muslim
  Bin Zubeiry Sports – Online: Timu nyingine ulizochezea za mtaani ni zipi                        
  Mbaraka Yussuf: Hakuna                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Ndondo ulikuwa huendi kupiga
  Mbaraka Yussuf: Siyo sana                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Simba uliingia lini
  Mbaraka Yussuf: Mwaka 2014                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Ulicheza timu B tu, au uliwahi kupandishwa?                        
  Mbaraka Yussuf: Nilicheza B, nikapandishwa timu kubwa, nikajiandaa nao pre season kule Lushoto (mwaka juzi). Nikaenda nao Zanzibar, kabla Ligi kuunza ndiyo wakanipeleka Kagera kwa mkopo ambako nilianza kucheza msimu uliopita, mkopo ukaisha msimu huu nimesaini mkataba wangu mwenyewe sasa 
  Bin Zubeiry Sports – Online: Unawakumbuka uliokuwa nao Simba B ambao nao sasa hivi wanawika Ligi Kuu
  Mbaraka Yussuf: Labda ninamkumbuka mmoja yule kipa Dennis (Richard) yeye ndiyo yupo SImba sasa hivi timu kubwa nay eye. Wengine sijui wapo timu gani kwa sasa 
  Bin Zubeiry Sports – Online: Umewahi kuchezea timu za vijana za taifa?                        
  Mbaraka Yussuf: Hapana                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Kwa Sasa unachuana na akina na Msuva na Kichuya kwenye mbio za ufungaji bora wa Ligi Kuu, unadhani utaweza kuwapiku hao?
  Mbaraka Yussuf: Hakuna jambo lisililowezekana. Cha muhimu ni juhudi tu. Kama siyo msimu huu, basi msimu mwingine nitajaribu tena.
  Bin Zubeiry Sports – Online: Unaonekana una mwili mdogo na mabeki wengi wa kati wameshiba shiba, unawezaje kufunga dhidi yao                        
  Mbaraka Yussuf: Ukiwa na Malengo na ukijituma unaweza kufunga dhidi ya beki yoyote hata mwili nyuma 
  Bin Zubeiry Sports – Online: Nini Ndoto zako katika soka 
  Mbaraka Yussuf: Kufika mbali zaidi                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Una Meneja?                        
  Mbaraka Yussuf: Sina Meneja                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Nani sasa anakufanyia mipango ya kufika mbele                        
  Mbaraka Yussuf: Ndiyo natafuta       
  Bin Zubeiry Sports – Online: Baada ya kufunga goli ukiichezea timu ya taifa (Taifa Stars) kwa mara ya kwanza Machi 28, timu nyingi zimevutiwa na wewe hapa nchini, je upo tayari kuondoka Kagera?   Mbaraka Yussuf: Yah Nipo tayari kuondoka Kagera                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Huna mkataba unaokubana?
  Mbaraka Yussuf: Sina                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Na unataka dau gani kuondoka Kagera
  Mbaraka Yussuf: Hiyo ni siri yangu                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Mama yako yuko wapi  
  Mbaraka Yussuf: Yupo Tandika                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Anafanya shughuli gani  
  Mbaraka Yussuf: Mfanyabiashara                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Mpo watoto wangapi kwenu 
  Mbaraka Yussuf: Kwenye familia tupo wawili tu, mimi na mdogo wangu wa kike, anaitwa Hanifa      
  Bin Zubeiry Sports – Online: Umri wake                        
  Mbaraka Yussuf:  Miaka 16                        
  Bin Zubeiry Sports – Online: Anafanya nini kwa sasa yeye
  Mbaraka Yussuf: Yupo tu nyumbani  
  Bin Zubeiry Sports – Online: Niseme kwa leo inatosha. Asante sana ninakutakia kila la heri
  Mbaraka Yussuf Abeid: Asante sana kaka. Nawe pia
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBARAKA YUSSUF: CHIPUKIZI MWENYE NDOTO ZA KUFIKA MBALI KISOKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top