• HABARI MPYA

  Sunday, May 07, 2017

  SERENGETI BOYS WAWASILI SALAMA GABON TAYARI KUKINUKISHA “MPAKA KOMBE LA DUNIAA”

  Na Mwandishi Wetu, LIBREVILLE
  KIKOSI cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kimewasili salama mjini Libreville nchini Gabon leo asubuhi tayari kwa Fainali za Afrika nchini humo kuanzia wiki ijayo.
  Serengeti Boys imewasili Gabon ikitokea Cameroon ambako ilikuwa kambi ya wiki moja na kucheza michezo miwili ya kujipima nguvu dhidi ya wenyeji, ikishinda moja 1-0 na kufungwa moja 1-0 pia.
  Vijana hao, walipokewa na Pellegrinius ‘Pelle’ Rutayuga, Mshauri wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ambaye alitangulia huko kuandaa mazingira ya timu kufikia na usalama wake kwa ujumla. Wamefikia katika hoteli ⁠Nomad.
  Serengeti Boys baada ya kuwasili mjini Libreville nchini Gabon leo asubuhi tayari kwa Fainali za Afrika nchini humo kuanzia wiki ijayo

  Serengeti Boys ilikwenda Cameroon ikitokea mjini Rabat nchini Morocco ambako iliweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na michauno inayotarajiwa kuanza Mei 14 hadi 28.
  Pamoja na kambi ya mazoezi, Serengeti Boys ikiwa mjini Rabat, Morocco ilicheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Gabon na kushinda 2-1 kila mchezo.
  Awali Serengeti Boys iliifunga Burundi mara mbili, Machi 30 mabao 3-0 na Aprili 1 mabao 2-0, mechi zote mbili zikipigwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Ghana ‘Black Starlets’ Aprili 3 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kikosi cha Serengeti Boys kilichotua Gabon kinaundwa na Makipa: Ramadhan Kabwili, Samwel Edward na Kelvin Kayego. 
  Mabeki: Kibwana Ally Shomari, Nickson Kibabage, Israel Mwenda, Dickson Job, Ally Msengi, Issa Makamba na Enrick Vitalis Nkosi. 
  Viungo: Kelvin Nashon Naftali, Ally Ng’anzi, Mohamed Rashid, Shaaban Ada, Mathias Juan, Marco Gerald, Abdulhamis Suleiman, Saidi Mussa na Cyprian Benedictor Mtesigwa.
  Washambuliaji:  Muhsin Malima Makame, Yohana Mkomola, Ibrahim Abdallah, Assad Juma na Abdul Suleiman.
  Benchi la Ufundi linaundwa na Bakari Shime (Kocha Mkuu), Oscar Mirambo (Kocha Msaidizi), Muharami Mohamed (Kocha wa makipa), Kim Poulsen (Mshauri wa Ufundi), Edward Evans (Mtunza Vifaa) na Shecky Mngazija (Daktari wa timu).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS WAWASILI SALAMA GABON TAYARI KUKINUKISHA “MPAKA KOMBE LA DUNIAA” Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top