• HABARI MPYA

  Sunday, May 07, 2017

  AZAM KUMUONGEZEA MKATABA KOCHA WAKE MROMANIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Azam FC imekubali kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja kocha wake mkuu, Mromania Aristica Cioba.
  Cioba ambaye alipewa jukumu la kukino kikosi cha timu hiyo mwanzoni mwa mwaka huu kwa mtabata wa miezi sita ambao unaishi mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online jana, Mwenyekiti wa timu hiyo, Nassor Idrissa ' Father' amesema wamekutana na kocha huyo baada ya kumalizika kwa mechi yao na Simba kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya.
  Azam FC imekubali kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja kocha wake mkuu, Aristica Cioba

  Alisema tayari Cioba amekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja ambapo ataendelea kukinoa kikosi hicho kwa msimu mwingine ujao.
  "Tulikutana na Kocha wetu, tukamsikiliza kama yupo tayari kuendelea na sisi au laa, amekubali hivyo baada ya kumalizika kwa ligi atasaini mkataba mpya," alisema Father.
  Alisema suala la wachezaji ambao wamemaliza mikataba yao wapo katika mazungumzi akiwemo Gadiel Michael. 
  " Kuhusu wachezaji wa kigeni hilo lipo kwa benchi la ufundi, kwani tunasubiri mapendekezo ya mwalimu kama kuna wachezaji atawahitaji tutaendelea nao na wale ambao hapo katika mipango yake watatusamehe," alisema Mwenyekiti huyo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM KUMUONGEZEA MKATABA KOCHA WAKE MROMANIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top