• HABARI MPYA

  Wednesday, May 03, 2017

  MSONDO NA SIKINDE ULINGONI MEI 20 MAGOMENI

  Na Mwandishi Wetu, Dar ss Salaam     
  BAADA ya kutafuta kwa muda wa miaka miwili hatimaye bendi hasimu za Msondo Ngoma na DDC Mlimani Park ‘Sikinde Ngoma ya Ukaye’ wanatarajia kuamua tena swali la nani zaidi kati yao.
  Katika pambano linalotarajia kufanyika Mei 20 Mwaka huu, katika ukumbi wa Traventine Magomeni, Dar es Salaam bendi hizo zinatarajiwa kushindana kwa umahiri wa kuporomosha burudani ya muziki mzuri.
  Mratibu wa pambano la Msondo na Sikinde, Abdulfareed Hussein  akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam leo. Na chini akiwatambulisha baadhi ya wanamuziki wa bendi hizo 
  Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam leo mratibu wa mpambano huo, Abdulfareed Hussein alisema mpambano huo wa nani zaidi utamuliwa na mashabiki wa dansi.
  Alisema kiingilio cha pambano hilo itakuwa ni Sh. 10,000 ili kuwapa nafasi wadau wa dansi kushuhudia na kutoa maamuzi ya nani zaidi kati ya bendi hizo mbili.
  "Hili pambano ndio litakata mzizi wa fitna, ambapo mashabiki ndio wataamua nani zaidi kati ya Msondo au Sikinde," alisema.
  Wakati huo huo: Mmoja wakilishi wa Sikinde, Abdallah Hemba alisema wamejiandaa vizuri kutoa burudani na kuhakikisha kwamba wako vizuri kuliko Msondo.
  “Hawa jamaa wametukimbia sana, hivyo kila tunapotaka kukutana nao wanakuwa na safari naona Mei 20 ndio mwisho wao," alisema.
  Nao Meneja wa Msondo, Said Kibiriti alisema wamejiandaa vyema hivyo katika pambano hilo wataimba nyimbo mchanganyiko
  “Tutaimba nyimbo mchanganyiko, pia tutaimba nyimbo zetu mpya, tunaamini mpambano huo ndio utaweza kuamua nani kati yao ni zaidi," alisema Kibiriti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSONDO NA SIKINDE ULINGONI MEI 20 MAGOMENI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top