• HABARI MPYA

    Monday, May 01, 2017

    MAALOUL APEWA TENA UKOCHA TIMU YA TAIFA TUNISIA

    KOCHA Nabil Maaloul Alhamisi aliteuliwa tena kuiongoza Tunisia kwa mara ya pili, miaka minne baada ya kufanya kazi hiyo kwa muda wa miezi saba.
    Mtu mzima huyo wa umri wa miaka 54, ambaye aliiongoza klabu ya Esperance ya Tunisia kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2011, anachukua nafasi ya Henryk Kasperczak aliyejiuzulu April.
    Taarifa ya Shirikisho la Soka Tunisia (FTF) imesema kwamba uteuzi huo unaanza mara moja.
    Maaloul alikuwa kocha wa timu ya taifa Februari mwaka 2013, lakini akajiuzulu baadaye mwaka huo.
    Kasperczak aliondoka baada ya Tunisia kutolewa kwenye Robo Fainali za Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Januari mwaka huu nchini Gabon.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAALOUL APEWA TENA UKOCHA TIMU YA TAIFA TUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top