• HABARI MPYA

  Tuesday, May 09, 2017

  KASEJA ANAANZA LEO KAGERA DHIDI YA YANGA TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MLINDA mlango mkongwe nchini, Juma Kaseja leo anaanza katika lango la Kagera Sugar kwenye mchezo dhidi ya timu yake ya zamani, Yanga SC.
  Kagera Sugar watakuwa wageni wa Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Saa 10:30 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Na misimu miwili tangu aondoke Jangwani, Kaseja atacheza dhidi ya Yanga kwa mara ya pili leo, baada ya Desemba 26 mwaka juzi kuidakia Mbeya City ikifungwa 3-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Juma Kaseja leo anaanza katika lango la Kagera Sugar dhidi ya timu yake ya zamani, Yanga SC

  Vikosi vya leo vipo hivi; Yanga SC; Benno Kakolanya, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa na Geoffrey Mwashiuya.
  Katika benchi wapo; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Vinecnt Bossou, Matheo Anthony, Deus Kaseke, Emmanuel Martin na Said Juma ‘Makapu’.
  Kagera Sugar; Juma Kaseja, Godfrey Taita, Mwaita Gereza, Babu Ali Seif, Mohammed Fakhi, George Kavilla, Suleiman Mangoma, Ally Nassor ‘Ufudu’, Mbaraka Yussuf, Ame Ali ‘Zungu’ na Edward Christopher.
  Katika benchi wapo; John Mwenda, Japhet Makarai, Themi Felix, Juma Jabu, Paul Ngway, Ali Ramadhani ‘Kagawa’ na Anthony Matogolo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KASEJA ANAANZA LEO KAGERA DHIDI YA YANGA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top