• HABARI MPYA

  Wednesday, May 10, 2017

  JUVE YATANGULIA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA,

  Beki wa kulia Mbrazil, Dani Alaves akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Juventus bao la pili dakika ya 44 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Monaco usiku wa Jumanne kwenye mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Juventus mjini Torino. Bao la kwanza la Juve lilifungwa na Mario Mandzukic dakika ya 33 wakati la Monaco limefungwa na Kylian Mbappe dakika ya 69 na kwa matokeo hayo Kibibi Kizee cha Turin kinakwenda fainali itakayopigwa mjini Cardiff kwa ushindi wa jumla wa 4-1, baada ya wiki iliyopita kushinda 2-0 Ufaransa na itapambana na mshindi wa jumla kati ya Real Maedrid na Atletico Madrid, zote za Hispania. Timu hizo zitarudiana kesho Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid baada ya mchezo wa kwanza Real Madrird kushinda 3-0 Uwanja wa Bernabeu, mabao yote akifunga Cruistiano Ronaldo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JUVE YATANGULIA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA, Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top