• HABARI MPYA

    Tuesday, May 09, 2017

    FIFA KUCHUNGUZA UHAMISHO WA POGBA KWENDA MAN UNITED

    SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limethibitisha mpango wa kuchunguza uhamisho wa Pauni Milioni 89.3 za kiungo Paul Pogba kutoka Juventus kwenda Manchester United msimu huu.
    Bodi ya Sheria ya FIFA imewasiliana na United kuomba ufafanuzi kutoka Old Trafford ikiwemo juu ya madai kwamba wakala wa Pogba, Mino Raiola amevuna kiasi cha Pauni Milioni 41 katika dili hilo.
    Inadaiwa mchezo mchafu umefanyika katika uhamisho wa wachezaji wote, Pogba na Zlatran Ibrahimovic aliyetua United pia msimu huu.

    FIFA inafanyia uchunguzi uhamisho wa Paul Pogba kwenda Manchester United kutoka Juventus PICHA ZAIDI GONGA HAOA


    Taarifa za ndani kutoka FIFA zimesema kwamba kwa muda sasa United imeombwa kutoa ufafanzi wa hatua za mwisho za usajili wa Pogba.
    Inafahamika kwamba, makubaliano ya Raiola na Juventus kupata asilimia 50 katika usajili wowote utakaozidi dau la Pauni Milioni 40 unavunja kanuni za umiliki wa mmiliki wa mtu tatu.
    Msemaji wa United ssmesema; "Hatuzungumzii mikataba, FIFA ilikuwa na makabrasha tangu uhamisho ulipokamilishwa Agosti mwaka jana.'
    Makabrasha yote yanapaswa kupitishwa kwenye mfumo wa usaili wa  FIFA na hayakuwahi kuonyesha tatizp lolote hadi sasa. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FIFA KUCHUNGUZA UHAMISHO WA POGBA KWENDA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top