• HABARI MPYA

  Friday, May 05, 2017

  HIMID MAO AENDELEZA MAKAMUZI DENMARK, WAZUNGU WAMKUBALI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA Msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Himid Mao ‘Ninja’, anaendelea na majaribio yake kwenye kikosi cha Randers inayoshiriki Ligi Kuu nchini Denmark.
  Himid tayari ameshafanya mazoezi mara mbili juzi na jana akiwa na kikosi cha wachezaji wa akiba wa timu hiyo, ambapo leo Jumatano alipewa mapumziko kabla ya kesho Ijumaa kuanza rasmi kujifua na kikosi cha kwanza cha Randers.
  Himid Mao ‘Ninja’, anaendelea na majaribio yake kwenye kikosi cha Randers inayoshiriki Ligi Kuu nchini Denmark

  Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, umeeleza kuwa kiungo huyo nyota mkabaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, 24, yuko tayari kwa mara ya kwanza kucheza soka la kulipwa na kulipa kisogo soka la nyumbani kwa kuhakikisha anapata mkataba wa kusajiliwa na Randers.
  Nyota huyo ambaye atafanya majaribio ndani ya timu hiyo kwa siku 10, aliondoka nchini Jumatatu iliyopita baada ya pande zote mbili za timu hizo kufanya makubaliano kuhusu mchezaji huyo, ambapo mara baada ya kumaliza zoezi hilo atarejea mara moja Azam FC kabla ya taratibu nyingine kufuata kama watakuwa wamevutiwa na huduma yake.
  Habari njema ni kuwa mbali na kufanya mazoezi na Randers, pia anatarajia kucheza mchezo mmoja akiwa na kikosi cha wachezaji wa akiba wa Randers kitakachocheza na AC Horsens Jumanne ijayo kwenye Ligi ya Wachezaji wa Akiba ndani ya Ligi Kuu ya Taifa hilo 'Danish Superliga'.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HIMID MAO AENDELEZA MAKAMUZI DENMARK, WAZUNGU WAMKUBALI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top