• HABARI MPYA

    Wednesday, May 03, 2017

    CAMEROON WALIPA KISASI KWA SERENGETI BOYS, WAIGONGA 1-0 NA WAO

    Na Mwandishi Wetu, YAOUNDE
    TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo imefungwa 1-0 na wenyeji Cameroon katika mchezo wa kirafiki mjini Yaounde, Cameroon.
    Kipigo hicho ni sawa na kisasi, baada ya Serengeti Boys kuifunga Cameroon 1-0 Aprili 30 katika mchezo mwingine wa kujipima nguvu.
    Siku hiyo, bao la Serengeti Boys lilifungwa na Ally Ng'anzi dakika ya 36 katika mchezo ambao ulihudhuriwa na gwiji wa soka wa Cameroon, Rogger Milla.
    Serengeti Boys ilitua Younde, Cameroon Alhamisi iliyopita ikitokea mjini Rabat, Morocco ambako iliweka kambi ya karibu mwezi mmoja na kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Gabon na kushinda 2-1 kila mchezo.
    Katika mechi saba za kujipima nguvu, Serengeti Boys imefungwa moja, sare moja na kushinda tano 
    Kwa ujumla Serengeti Boys imekwishacheza mechi sita tangu kuanza kambi rasmi ya maandalizi fainali za Gabon, baada ya awali kuifunga Burundi mara mbili, Machi 30 mabao 3-0 na Aprili 1 mabao 2-0, mechi zote mbili zikipigwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Ghana ‘Black Starlets’ Aprili 3 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Baada ya mchezo wa leo, Serengeti Boys inatarajiwa kuendelea na mazoezi katika kambi yake ya wiki moja Cameroon, kabla ya Mei 7 kwenda Gabon ambako imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola.
    Cameroon nayo itashiriki fainali hizo ikiwa imepangwa Kundi A lina timu za wenyeji, Gabon, Guinea na Ghana. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAMEROON WALIPA KISASI KWA SERENGETI BOYS, WAIGONGA 1-0 NA WAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top