• HABARI MPYA

    Monday, September 19, 2016

    SABABU KWA NINI ULIMWENGU HAKUCHEZA TP MAZEMBE JUMAMOSI NA TAYARI YUPO DAR

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu ameshindwa kusafiri na timu yake, TP Mazembe ya DRC kwenda Tunisia kutokana na pasipoti yake kwisha.
    Mazembe ilibisha hodi Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kulazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya wenyeji, Etoile du Sahel Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia usiku wa Jumamosi.
    Na Ulimwengu hakusafiri na mabingwa hao wa mwaka jana Afrika kutokana na kulazimika kurejea nyumbani kushughulikia pasipoti mpya.

    Thomas Ulimwengu amerejea nyumbani kushughulikia pasipoti 

    “Nipo nyumbani kushughulikiwa pasipoti mpya, natarajiwa kufanikisha mpango huu ndani ya siku mbili hizi na nikiipata mara moja narejea Lubumbashi,”amesema Ulimwengu. 
    Jumamosi wenyeji walitangulia kwa bao la kiungo Hamza Lahmar dakika ya 20, kabla ya Rogger Assale kuisawazishia Mazembe dakika ya 52.
    Mazembe sasa watahitaji hata sare ya 0-0 katika mchezo wa marudiano nyumbani Septemba 25 mjini Lubumbashi ili kwenda fainali, ambako watakutana na mshindi wa jumla kati ya Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria na FUS Rabat ya Morocco.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SABABU KWA NINI ULIMWENGU HAKUCHEZA TP MAZEMBE JUMAMOSI NA TAYARI YUPO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top