• HABARI MPYA

  Sunday, April 10, 2016

  TP MAZEMBE YACHEZEA 2-0 ZA WYDAD

  TP Mazembe imeweka rehani taji la Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kufungwa mabao 2-0 na wenyeji Wydad Casablanca katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora mjini Marrakech, Morocco usiku wa Jumamosi.
  Mabao ya Wydad yamefungwa na Noussir Abdellatif dakika ya 44 na Reda Hajhouj dakika ya 66 kwa penalti.
  Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu aliingia dakika ya 58 kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba na akaipa misukosuko ya kutosha ngome ya Wydad.

  Mazembe sasa inatakiwa kushinda 3-0 wiki ijayo nyumbani Lubumbashi ili kufufua matumaini ya kutetea taji lake.
  Mechi nyingine za kwanza 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Jumamosi, Zesco United ya Zambia imeshinda 3-1 dhidi ya Stade Malien Uwanja wa Modibo Keita, Zamalek imeshinda  2-0 dhidi ya MO Bejaia ya Algeria Uwanja wa Petro Sport, El Merreikh imelazimishwa sare ya 2-2 ES Setif ya Algeria Uwanja wa El Merriekh mjini Khartoum,
  Asec Mimosas kimeshinda 2-0 dhidi ya Ahly Tripoli ya Libya Uwanja wa Robert Champroux mjini Abidjan na Yanga SC imelazimishwa sare ya 1-1 na Al Ahly ya Misri Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TP MAZEMBE YACHEZEA 2-0 ZA WYDAD Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top