• HABARI MPYA

    Friday, October 02, 2015

    KIIZA BADO SI SHWARI SIMBA SC, DAKTARI ASEMA…

    MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA Oktoba 3, 2015
    Mgambo Shooting Vs Coastal 
    Majimaji FC Vs Mwadui FC
    Toto Africans Vs JKT Ruvu
    Stand United Vs Mbeya City
    Kagera Sugar Vs Prisons Kaitaba
    Oktoba 17, 2015
    Yanga SC Vs Azam Fc
    Majimaji FC Vs African Sports
    Mbeya City Vs Simba Sc Sokoine
    Ndanda FC Vs Toto Africans
    Stand United Vs Prisons
    Coastal Union Vs Mtibwa Sugar
    Mgambo Shooting Vs Kagera Sugar 
    Mwadui FC Vs JKT Ruvu
    Majibu ya vipimo vya mshambuliaji wa Simba SC, Hamisi Kiiza 'Diego' yanatarajiwa kutoka leo

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC leo inatarajiwa kujua itamkosa kwa muda gani, mshambuliaji wake tegemeo la mabao, Mganda Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’.
    Kiiza aliumia mazoezini mapema wiki hii, Simba SC ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Stand United juzi, wakishinda 1-0, bao pekee la Joseph Kimwaga.
    Na Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kwamba majibu ya vipimo vya Kiiza yatatoka leo.
    “Majibu yake (Kiiza) tutayapata Ijumaa na ndiyo tutajua anahitaji kupumzika kwa muda gani,”amesema Gembe, ambaye awali alikuwa Daktari wa timu nyingine ya Ligi Kuu, Mtibwa Sugar.
    Kiiza aliyueumia nyama za paja, hadi sasa ndiye kinara wa mabao wa Simba SC katika Ligi Kuu akiwa amefunga mabao matano katika mechi nne alizocheza.
    Baada ya kupoteza mchezo mmoja tu katika mechi tano, nyingine zote ikishinda, Simba SC itarudi kwenye Ligi Kuu Oktoba 17, itakapomenyana na Mbeya City mjini Mbeya.
    Lakini Ligi Kuu itaendelea kesho bila kuzihusisha Azam FC, Simba na Yanga SC, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Mgambo Shooting wakimenyana na  Coastal Union, Uwanja wa Majimaji, Songea wenyeji Majimaji FC wakiwakaribsiha Mwadui FC, Uwanja wa CC,m Kirumba,  Toto Africans wakiikaribisha  JKT Ruvu, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga Stand United wakiikaribisha Mbeya City na Uwanja wa A.H. Mwinyi, Tabora, Kagera Sugar wakiikaribisha Prisons.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIIZA BADO SI SHWARI SIMBA SC, DAKTARI ASEMA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top