TIMU ya Singida Black Stars imetoa sare ya bila mabao na wenyeji, Stellenbosch katika mchezo wa mwisho wa Kundi C Kombe la Shirikisho Afrika usiku huu Uwanja wa DHL Jijini Cape Town nchini Afrika Kusini.
Kwa matokeo hayo, Singida Black Stars inamaliza na pointi nne katika nafasi ya tatu ikiizidi tu wastani wa mabao Stellenbosch iliyoshika mkia.
Mechi nyingine ya mwisho ya kundi hilo, wenyeji CR Belouizdad wameichapa AS Otoho ya Jamhuri ya Kongo 2-1 Uwanja wa Nelson Mandela Jijini Algiers nchini Algeria.
Kwa matokeo hayo, CR Belouizdad imeongoza Kundi C kwa pointi zake 12 na AS Otohô iliyomaliza na pointi tisa na zote zimefuzu Robo Fainali.

.png)
0 comments:
Post a Comment