• HABARI MPYA

    Friday, February 06, 2026

    TANZANIA PRISONS YAAMBULIA SULUHU KWA MASHUJAA SOKOINE


    WENYEJI, Tanzania Prisons wamelazimishwa sare ya bila mabao na Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Kwa matokeo hayo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 10 katika mchezo wa 12, ingawa wanabaki nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 wakiizidi pointi mbili KMC inayoshika mkia ambayo pia ina mechi nne mkononi.
    Kwa upande wao Mashujaa FC baada ya sare hiyo wanafikisha pointi 15 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya nane kutoka ya tisa.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YAAMBULIA SULUHU KWA MASHUJAA SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top