TIMU ya Mtibwa Sugar imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mshambuliaji Cyprian Kipenye alianza kuifungia Namungo FC dakika ya 36, kabla ya kiungo Said Mkopi kuisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 44.
Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 21 katika mchezo wa 13 na kurejea nafasi ya tatu, wakati Namungo FC inafikisha pointi 20 katika mchezo w 12, ingawa inabaki nafasi ya tano.


.png)
0 comments:
Post a Comment