TANZANIA imeitoa Kenya katika mbio za kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya umri wa miaka 20 kufuzu Fainali za Kombe la Dunia kwa penalti 3-1 kufuatia sare ya jumla ya 1-1 kila timu ikishinda 1-0 nyumbani katika Raundi ya Tatu.
Mchezo Februari 7 Kenya ilishinda 1-0 Uwanja wa Ulinzi Sports Complex, Nairobi na katika marudiano Tanzania nayo imeshinda 1-0 jioni ya leo Uwanja Wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Hata hivyo, Tanzania ikafanikiwa kwenda Raundi ya Nne na ya mwisho ya mchujo huo kwa ushindi Wa penalti 3-1 na sasa itakutana na Cameroon mwezi Mei katika mechi nyingine mbili za nyumbani na ugenini.
Timu nne zitaiwakilisha Afrika katika Fainali za Kombe la Dunia la FIFA U20 Wanawake 2026 U-20 nchini Poland.

.png)
0 comments:
Post a Comment