• HABARI MPYA

    Saturday, February 07, 2026

    MBEYA CITY YAICHAPA TRA UNITED 2-0 PALE PALE TABORA


    TIMU ya Mbeya City imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
    Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Adili Willy Buha kwa penalti dakika ya 36 na Said Naushad Said dakika ya 74 katika mchezo ambao TRA United ilipata pigo la mapema kufuatia beki wake, Omary Yussuf Seif kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 19.
    Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi 13 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya 10 ikizidiwa tu wastani wa mabao na TRA United ambayo hata hivyo imecheza mechi 11 hadi sasa. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YAICHAPA TRA UNITED 2-0 PALE PALE TABORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top