TIMU ya Azam FC imechapwa mabao 2-0 na wenyeji, Wydad AC katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
Mabao ya Wydad Athletics Club yamefungwa na beki Paschal Gaudence Msindo aliyejifunga dakika ya 64 na mshambuliaji Mfaransa, Nassi Ouled Bentle dakika ya 90’+4'.
Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi B Kombe la Shirikisho, AS Maniema Union imeichapa Nairobi United FC mabao 3-0 Uwanjawa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kwa matokeo hayo Wydad inamaliza kileleni na pointi zake 15, ikifuatiwa na AS Maniema Union yenye pointi 12 na zote zinakwenda Robo Fainali, wakati Azam FC inamaliza na pointi tisa mbele ya Nairobi United ambayo imefungwa mechi zote na zote safari yao inaishia hapa.



.png)
0 comments:
Post a Comment