MWANARIADHA nyota wa Tanzania, Gabriel Geay ameendelea kupeperusha vyema bendera ya taifa baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mbio za Daegu Marathon zilizofanyika nchini Korea Kusini.
Geay aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa saa 2:08:05, akionesha kiwango cha juu cha ushindani, uthabiti na uzoefu mkubwa katika mbio za kimataifa.
Ushindi huo unamfanya kutetea ubingwa wake kwa mara ya pili mfululizo mafanikio yanayoendelea kumuweka katika ramani ya wanariadha bora duniani katika mbio za masafa marefu.
Geay pia anashikilia rekodi ya Taifa ya marathon (2:03:00) aliyoiweka mwaka 2023 katika mbio za Valencia Marathon, mafanikio yaliyoimarisha hadhi yake katika riadha ya kimataifa.
Hongera Gabriel Geay kwa ushindi huu mkubwa na kwa kuendelea kuiwakilisha Tanzania kwa mafanikio makubwa duniani.


.png)
0 comments:
Post a Comment