TIMU ya Simba SC imehitimisha mechi zake za Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi Wa 1-0 dhidi ya Stade Malien ya Mali usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Pongezi kwa mfungaji Wa bao hilo pekee la Simba SC katika mchezo huo, mshambuliaji Muivory Coast, Alain Anicet Oura dakika ya pili tu ya mchezo huo.
Ushindi huo wa kwanza kwenye hatua hiyo baada sare mbili awali na kufungwa mechi tatu unaifanya Simba ifikishe pointi tano, ingawa inamaliza mkiani mwa Kundi D.
Mchezo mwingine wa mwisho wa Kundi D leo, wenyeji Esperance Tunis wameichapa Petro Atletico ya Angola mabao 2-0 Uwanja wa Olimpiki Hammadi Agrebi mjini Radès nchini Tunisia.
Stade Malien imeongoza Kundi D kwa pointi zake 11 ikifuatiwa na Espérance iliyomaliza na pointi tisa na zote zinakwenda Robo Fainali, wakati Petro de Luanda ya Angola iliyomaliza na pointi sita nafasi ya tatu imetolewa kama Simba SC.

.png)
0 comments:
Post a Comment