• HABARI MPYA

    Friday, February 13, 2026

    MASHUJAA YAZINDUKA CHINI YA JULIO, YAICHAPA MTIBWA 3-1 DODOMA


    IKIONGOZWA na Kocha mpya kwa mara ya kwanza, Jamhuri Kihwelo 'Julio' timu ya Mashujaa FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
    Mabao ya Mashujaa FC yamefungwa na Hassan Ali dakika ya 37, Jaffar Salum Kibaya dakika ya 74 na Abdul Bakari dakika ya 90’+1, wakati la Mtibwa Sugar limefungwa na Charles Magata kwa penalti dakika ya 81.
    Kwa ushindi huo, Mashujaa FC inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 15 na kuruka hadi nafasi ya nane kutoka ya 10, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 21 za mechi 14 Sasa nafasi ya nne.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MASHUJAA YAZINDUKA CHINI YA JULIO, YAICHAPA MTIBWA 3-1 DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top