TIMU ya JKT Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Mshambuliaji Valentino Mashaka Kusengama alianza kuifungia JKT Tanzania kwa penalti dakika ya tatu, kabla ya winga mkongwe Shiza Ramadhani Kichuya kuisawazishia Coastal Union dakika ya 13.
Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 16 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, wakati Coastal Union imefikisha pointi 15 katika mchezo wa 15 ingawa inabaki nafasi ya tisa kwenye ligi ya timu 16.

.png)
0 comments:
Post a Comment