• HABARI MPYA

    Saturday, February 14, 2026

    TANZANIA PRISONS YAICHAPA NAMUNGO FC 3-2 SOKOINE


    WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Lambert Sabiyanka dakika ya 49, George Mpole kwa penalti dakika ya 71 na Oscar Mwajanga dakika ya 78, wakati ya Namungo FC yamefungwa na Cyprian Kipenye kwa penalti dakika ya 39 na Mkongo Fabrice Ngoy dakika ya 42. 
    Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 13 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 14 kwenye ligi ya timu 16, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 20 za mechi 14 sasa nafasi ya tano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YAICHAPA NAMUNGO FC 3-2 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top