TIMU ya Azam FC imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Maniema Union ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Bao pekee la Azam FC katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Mali, Sadio Kanoute dakika ya 24.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi tisa ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa tu wastani wa mabao na AS Maniema Union baada ya wote kucheza mechi tano.
Azam FC itamalizia ugenini na Wydad AC Februari 15 Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca nchini Morocco, wakati AS Maniema Union inarejea nyumbani kumaliza na Nairobi United Uwanja wa Martyrs Jijini Kinshasa siku hiyo pia.


.png)
0 comments:
Post a Comment